PICHA NA MAELEZO MACHACHE YA MTOTO ALIYECHOMWA MOTO NA KULAZIMISHWA KULA KINYESI.

 


BAADA ya kuchomwa moto katika mkono wake, kufungiwa ndani na kulazimishwa kula kinyesi chake, hatimaye mtoto Aneth (3) mkazi wa Majengo jijini hapa amekatwa mkono wake wa kushoto,

 
Mtoto Aneth (3) kabla ya kukatwa mkono.
Mapema wiki hii iliripotiwa kuwa, Aneth amekuwa akiteswa na mama yake mdogo, Bahati Rukangara kutokana na sababu ambazo hazijajulikana mpaka sasa.
Kwa mujibu wa majirani, Aneth alifungiwa ndani na mama yake huyo na kufanyiwa kitendo hicho ambacho wamekiita ni zaidi ya unyama.

“Tulilazimika kuvunja mlango na kumtoa Aneth kisha kumpeleka Hospitali ya Mkoa baada ya kumsikia akilia, uchunguzi ulipofanyika  madaktari wakaona ili kumponya wamkate mkono wake wa kushoto,” alisema jirani mmoja wapo.
“Mkono ulishaharibika, madaktari hawakuwa na budi kuukata, hivyo kumsababishia kilema cha maisha mtoto huyo wa watu,” aliongeza jirani mwingine aliyeguswa na tukio hilo.
 
...Baada ya kukatwa mkono.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Majengo, Habiba Mwakitalu amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuthibitisha kuwa Bahati anashirikiliwa na polisi kutokana na madai hayo ya unyanyasaji.
“Tulipomhoji Aneth alisema mama yake mdogo alikuwa akimfunga nguo mkononi na kumwagia maji ya moto, pia alisema alikuwa akilazimishwa kula kinyesi chake lakini alishindwa kuvumilia na kuanza kupiga kelele kwa lengo la kuomba msaada,” alisema Mwakitalu.
Gazeti hili limesikitishwa sana na kitendo alichofanyiwa mtoto huyo na linaomba vyombo vya dola vimshughulike mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Mama Mdogo wa Aneth, Bahati Rukangara.

Comments