ALIYEKUWA mshehereshaji katika Shindano la Miss Tanzania 2012, Jokate Mwegelo juzikati alijikuta akilizwa iPad yake ndani ya Ukumbi wa Cristal Palace uliopo kwenye Hotel ya Blue Pearl, Ubungo Plaza, jijini Dar.

Jokate Mwegelo.
Tukio hilo lilijiri wakati warembo
waliokuwa wakishiriki shindano hilo wakifanya ‘riheso’ ambapo Jokate
aliiacha iPad yake na kwenda kufanya majaribio ya kipaza sauti
alichotakiwa kukitumia.
“Jamani iPad yangu ilikuwa hapa mbona siioni, naomba aliyeichukua anirudishie, nataka kuondoka kwenda kujiandaa,” alisikika Jokate.
Baada ya kupita takriban nusu saa bila majibu, ndipo uvumilivu ulianza kumshinda mlimbwende huyo na kuanza kutokwa machozi baada ya kuona dalili za kurudishiwa hazikuwepo.
Mpaka Amani linatoka ukumbini hapo saa nane mchana, mrembo huyo hakufanikiwa kuiona iPad yake ambayo inakadiriwa kuuzwa kwa shilingi milioni moja za Kibongo.

Ipad.
Comments
Post a Comment