
MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’, amepatwa na kile kinachoonekana ni balaa nambari moja tangu apate umaarufu.
Gari la Diamond aina ya Toyota Land Cruiser Prado TX baada ya kugongana na Toyota Rav 4.
Jumamosi iliyopita, Diamond akiwa anaendesha gari lake la kifahari
aina ya Toyota Land Cruiser Prado TX, aligongana na Toyota Rav4,
lililokuwa linaendeshwa na mwanamke mmoja ambaye jina lake
halijapatikana.Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela, Diamond aligongana na mwanamke huyo kwenye Barabara ya Kimweri, Msasani, Dar es Salaam, saa 3 usiku.
Kenyela alisema, askari wa barabarani walichunguza na kubaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni pikipiki ambapo wakati Diamond anakata kona, alijaribu kuikwepa pikipiki hiyo ndipo akakutana uso kwa uso na Rav4 la mwanamke huyo.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’.
“Baada ya kugongana, gari la Diamond liliendelea kuserereka na
kuigonga pikipiki pamoja na aliyekuwa anaiendesha. Hakuna aliyefariki
kwenye ajali hiyo, wote walipata maumivu.”Kwa upande mwingine, ilibainika kuwa Diamond baada ya kupata ajali hiyo, alikwenda Hospitali ya TMJ kwa matibabu baada ya kujihisi amepatwa na maumivu.
Diamond hakupatikana ili kuzungumzia ajali hiyo lakini kwa kumbukumbu, kabla ya kumiliki gari hilo la kifahari aliwahi kumiliki magari mengine mawili, likiwemo lile alilokaa nalo kwa muda mrefu, Toyota Opa lakini hakuwahi kupata ajali ya kiwango hicho.

Comments
Post a Comment