
Kogelo, Kenya
LICHA ya ushindi wa Rais Barack Obama, nyuma ya pazia kuna taarifa kuwa, mzee mmoja ambaye ni mganga wa kienyeji aliyefahamika kwa jina la John Dimo (105) alimfanyia mambo ya kishirikina ili kumhakikishia ushindi.
Mganga
wa kienyeji aliyefahamika kwa jina la John Dimo anayedaiwa kumfanyia
mambo ya kishirikina Rais Obama ili kumhakikishia ushindi.
Inaelezwa kuwa, siku moja kabla ya matokeo ya uchaguzi mzee huyo
aliingia kwenye kijumba chake cha nyasi kilichopo Magharibi mwa Kenya
ambako ni nyumbani kwa baba wa Obama kisha akafanya ‘mandingo’ yake.“Baada ya kufanya ushirikina wake, alichukua majumba mawili ya konokono, moja akalipa jina la Romney na lingine jina la Obama kisha akatoka nje na kuyatupa mbali.
...Mganga John Dimo akiwa kazini.
“Baada ya zoezi hilo, akayafuata na kukuta lile alilolipa jina la
Obama liko mbele ya lile la Romney, akabaini kuwa ushirikina wake
umefanya kazi na ndipo alipowatangazia watu kuwa, Obama atashinda bila
kipingamizi,” alieleza jirani wa mzee huyo.
...Akionyesha ushindi wa Obama.
Hata hivyo, baada ya matokeo kutangazwa Jumatano iliyopita, mzee huyo
alijipatia umaarufu mkubwa na watu waliomfagilia licha ya wengine
kueleza kuwa, ushindi wa Obama umetokana na uchapakazi wake pamoja na
kupendwa na watu na si mambo ya ushirikina.
Rais Barack Obama
source GPL,
Comments
Post a Comment