YATIMA ALIYEUNGUA, AHAMISHIWA CCBRT

 
Na Mwandishi Wetu, Iringa
MTOTO yatima Juliana Mwinuka, mkazi wa Kijiji cha Mavanga, wilayani Ludewa, mkoani Njombe aliyeungua usoni baada ya kuangukia kwenye moto kutokana na maradhi yake ya kifafa, amehamishiwa katika Hospitali ya CCBRT akitokea Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Habari za mtoto huyo zilichapishwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika gazeti ndugu na hili la Amani.
Mtoto Juliana Inuka.
Mwandishi wa gazeti hili Francis  Godwin aliyemuibua mtoto huyo kijijini Mavanga, akiwa hana msaada wowote kutokana na ufukara wa mtu anayeishinaye alipozungumza jana na gazeti hili ameeleza sababu za kuhamishiwa katika hospitali hiyo.
“Amehamishiwa CCBRT kwa kuwa kuna taarifa kuwa kuna  madaktari bingwa kutoka nchi mbalimbali duniani watafika hapo kwa ajili ya kuwafanyia matibabu  wagonjwa tukaona ni vyema akapata bahati hiyo,” alisema Godwin.
Alipoulizwa hali yake kwa sasa ikoje, Godwin alisema: “Hali yake imeendelea  kuleta matumaini baada ya kuanza kukaa mwenyewe  huku akiweza kuinua mikono jambo ambalo  linazidi  kututia moyo.”
Alisema anawashukuru wale wote walioguswa na kutoa msaada kutokana na tatizo la mtoto huyo aliyeungua kwa kuangukia moto kutokana na kusumbuliwa na kifafa.
Wote walioguswa na habari ya mtoto huyu na kuwa na moyo wa kumsaidia wawasiliane na mratibu wa matibabu yake ambaye ni mwandishi wetu kwa namba hizi  M-pesa 0754 026 299 au Tigo Pesa 0712 750199.


SOURCE....GPL

Comments