
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), liliagiza Yanga imlipe Njoroge raia wa Kenya, Sh milioni 17 kutokana na kumuacha bila ya malipo. Akizungumza na Championi Ijumaa, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema suala la Njoroge kwa sasa limeisha katika ngazi ya Fifa ambapo limebaki katika ngazi ya klabu husika, ambayo itamlipa hadi pale deni litakapomalizika.
“Kwa sasa madai ya Njoroge yaliyokuwa Fifa yameisha baada ya kukamilika kwa taratibu ambapo Yanga wanamlipa kiasi cha shilingi milioni moja kila mwezi hadi deni lake litakapokamilika ikiwa ni pamoja na kumlipa kwa riba ya asilimia 5 kutokana na kuchelewesha.
“Suala pekee ambalo limebaki Fifa kwa sasa ni la Papic ambapo mchakato bado unaendelea,” alisema Wambura.
Upande wa Yanga, Kaimu Katibu Mkuu, Lawrance Mwalusako alipotakiwa kulitolea ufafanuzi suala hilo, alisema hawezi kulizungumzia kwa kuwa masuala yanayohusiana na fedha yanawahusu viongozi wa juu zaidi.
Comments
Post a Comment