WAZIRI MKUU AONGOZA MAANDAMANO YA KUIPINGA SERIKALI NCHINI INDIA KWA UAMUZIWAKE

Zaidi ya watu elfu moja wamefanya maandamano katika mji
mkuu wa India , Delhi, wakipinga uamuzi wa serikali kuruhusu makampuni ya kigeni kuekeza katika biashara za masoko makubwa.
Maandamano hayo, yaliongozwa na waziri mkuu wa jimbo la Bengal,Magharibi Mamata Banerjee.
Chama chake cha kisiasa Trinamool Congress, hivi karibuni kiliwaondoa mawaziri wake kutoka kwa serikali ya taifa kuonyesha upinzani wake kuhusu sera hiyo.
Serikali imakubali kuruhusu maduka makubwa ya kifahari ya kigeni kufanya kazi nchini humo kwa ushirikiano na maduka ya nchini humo ingawa yatakuwa na umiliki mkubwa kuliko maduka ya nyumbani.

Comments