
Mhubiri mmoja wa kiisilamu katika kijiji cha Izbat Marco, alisema kuwa aliwaona vijana hao wenye umri wa miaka tisa na kumi wakirarua nakala za Koran na kisha kuzikojolea.
Kasisi wa kikopti, alisema kuwa waandamanaji kijijini humo walifanya maandamano kutaka waombwe msamaha kwa kosa hilo.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yanasema kuwa kesi za kuidhihaki dini zimeongezeka mno.
Kesi kumi na saba zimefikishwa mahakamani, tangu vurugu za mwaka 2011 nyingi zikiwa dhidi ya wakristo wakopti, ambao idadi yao ni asilimia kumi na tatu ya watu milioni 82 nchini humo.
Hali ya sintofahamu ilizuka mwezi jana baada ya mkristo mkopti kutoa kanda ya video iliyomdhihaki Mtume wa kiisilamu Muhammad pamoja na dini na kusababisha ghasia na vurugu katika nchi za kiisilamu kote duniani.
Jirani wa vijana hao aliwapa hifadhi na kusema kuwa alishuku madai hayo kuwa ya kweli kwa sababu ni ya kushangaza na kwamba watoto hao hawakuweza kutambua Quran.
"Nilimuuliza mtoto mmoja ikiwa aliijua Quran na ikiwa aliweza kuitambua. Hakujua kama ilikuwa Quran, hawezi hata kuandika wala kusoma kama watoto wengine vijijini'' mtu huyo alikunuliwa akiambia shirika la habari la Associated Press.
Polisi waliwazuilia watoto hao kwa ajili ya usalama wao, kwa sababu waisilamu wenye msimamo mkali walikusanyika katika msikiti wakitaka kulipiza kisasi.
Comments
Post a Comment