WATOTO 18 WAFARIKI PAPO HAPO BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI

Maafisa wa utawala nchini China, wameanzisha uchunguzi wa vifo vya watoto 18 wa shule moja ya msingi nchini humo.

Watoto hao walifukiwa na vifusi baada ya maporomoko ya ardhi kutokea Kusini Magharibi mwa nchi.
Meya wa mji wa Shaotong, Liu Jianhua, alisema kuwa uchunguzi unafanywa kubaini ikiwa kuna mtu wa kulaumiwa kwa tukio hilo.
Waokoaji wameweza kupata mwili wa mwisho kutoka kwenye vifusi hivyo.
Watoto walikuwa wakitumia madarasa yaliyokuwa yamekodiwa kutoka kwa shule jirani kwa lengo la kufanya masomo ya ziada wakati wa kipindi cha likizo.
Shule yao iliharibiwa kufuatia tetemeko la ardhi mwezi jana.

Comments