WAPIGWA MIAKA 5 GEREZANI KWA KULA RUSHWA

Mawakala wawili wa tume ya kupambana na ufisadi, wamehukumiwa miaka mitano kila mmoja gerezani kwa kupokea rushwa.

Tume ya kupambana na ufisadi nchini humo, imesema kuwa maafisa wake walipatikana na hatia baada ya kuchukua rushwa ya kiasi i cha dola 390 kutoka kwa mwanasiasa ili wasitishe uchunguzi uliokuwa unaendelea.
Shirika la kupambana na ufisadi nchini humo limekuwa likikosolewa kwa namna linavyofanya kazi zake, kukabiliana na kile ambacho baadhi wanasema ni viwango vya juu vya ufisadi.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yanasema kuwa tume hiyo iliyoundwa mwaka 2002 - miaka mitatu baada ya utawala wa kijeshi, imekuwa likiingiliwa kisiasa.
Katika taarifa yake tume ya EFCC, Douglas William na Abba Ishaku walikamatwa mwaka 2010, baada ya kujaribu kupokea rushwa kutoka kwa mwenyekiti wa baraza la miji katika jimbo la Borno,Kullima Kachalla.
Mawakala hao walimhadaa kwa kumwambia mwanasiasa huyo kuwa wataweza kuharibu nyaraka zilizonuiwa kutumiwa kuanzisha uchunguzi kuhusu kashfa ya ubadhirifu wa mali ya umma dhidi yake.

Comments