WANACHI WAVAMIA BUNGE LIBYA

Waandamanaji wamevamia bunge nchini Libya kupinga orodha jipya la mawaziri

Waandamanaji hao wametoka katika miji ya Zawiya na Zuwara, maeneo ambayo wanasema hayana uwakilishi sawa katika orodha ya baraza hilo jipya la mawaziri.
Wabunge nchini humo, wanajadili orodha ya mawaziri walioteuliwa mnamo siku ya Jumatano na waziri mkuu Mustafa Abushagur.
Wengi wamekosoa orodha hiyo kwa kukosa mawaziri kutoka kwa vuguvugu la waliberali

Comments