UN: IDADI YA WAZEE INAONGEZEKA KWA KASI KULIKO WATU WENYE UMRI MWINGINE DUNIANI

Umoja wa Mataifa unasema kuwa idadi ya watu wakongwe inaongezeka kuliko watu wenye umri mwingine wowote duniani na kwamba hali hii
inahitaji kudhibitiwa hasa katika nchi zinazostawi.
Ripoti moja iliyotolewa na shirika la Umoja huo la kukadiria idadi ya watu duniani, inakariri kwamba, katika kipindi cha miaka kumi iyajo, idadi ya watu wataokuwa na zaidi ya umri wa miaka sitini itawadia bilioni moja.
Shirika la kuwahudumia wakongwe, la Help Age,ambalo limechangia ripoti hiyo, linatoa hamasa kwa nchi mbali mbali kuanzisha hazina bora zaidi za malipo ya uzeeni.
Ripoti hiyo inasema mikakati yenye mwelekeo mzuri kuhusu afya na ajira itahitajika ili kuimarisha hazina hizo.

Comments