UMOJA WA ULAYA WAITAKA KAMPUNI YA GOOGLE KUBADILI UTENDAJI WA KAZI ZAKE

Muungano wa Ulaya umeitaka kampuni ya Google kubadili utenda kazi wake hasa inavyokusanya taarifa za faragha kuhusu watu ili kulinda taarifa muhimu za watumiaji wa mitandao yake.

Wadhibiti wa taarifa za faragha za watu barani Ulaya, wanatishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kampuni hiyo ikiwa Google itakataa kuweka wazi sera yake kuhusu ukusanyaji wa taarifa za faragha za watu kuhakikisha inaambatana na sheria za ulaya katika kipindi cha miezi michache ijayo.
Wana wasiwasi kuhusu sera mpya ya kampuni hiyo iliyotolewa mwezi Machi ambayo inaruhusu kampuni hiyo kukusanya taarifa ambazo mtandao wake wa kijamii wa Youtube na ule wa barua pepe, Gmail zinatumia kuhusu watu.
Wadhibiti wanasema kuwa Google haitoi maelezo ya kina kuhusu taarifa inazokusanya kuhusu watu, ambavyo inatumia taarifa hizo na kwa muda gani inanuia kuzihifadhi taarifa hizo.
Hata hivyo Google imesisitiza kuwa sera zake zinaambatana na sheria za ulaya.

Comments