
Makubalino hayo na kundi la Moro Islamic Liberation Front (MILF), yanakusudiwa kuanzisha eneo la Waislamu litalokuwa na madaraka ya kadiri fulani kusini mwa nchi, linaloitwa Bangsamoro.
MILF imesema imefurahi sana na Rais Benigno Aquino alisisitiza kuwa mpango huo unajumuisha makundi yote yaliyotaka kujitenga.
Lakini ukubwa wa eneo hilo jipya la Waislamu hujulikani, na lazima mpango huo ukubaliwe kwa kura ya maoni ya wananchi ambao wengi wao ni Wakatoliki.
Comments
Post a Comment