UCHUMI WA UINGEREZA HATARINI

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, ameonya kuwa Uingereza itaanguka kiuchumi na kuvuta mkia nyuma ya Brazil, China na India iwapo haitapunguza nakisi ya bajeti yake na kuwa ya ushindani zaidi.

Bw Cameron ameuambia mkutano mkuu wa kila mwaka wa chama chake cha Conservative kuwa Uingereza inaweza kukabiliana na changamoto hiyo kwa kuimarisha elimu yake, kupunguza matumizi katika ustawi wa jamii na kuamusha ari miongoni mwa watu wake.
Ingawa ilikuwa inachukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa kutibu uchumi wake urejee kwenye kukua tena, Cameron amesema nakisi ya taifa imepunguzwa kwa kiasi cha robo katika miaka miwili iliyopita.

Comments