Kikosi cha Toto African.

HUKU ikiwa na maumivu ya kufungwa bao 1-0 mjini Bukoba, Yanga imepokea taarifa nyingine kwamba Mwanza haitatoka salama.
Kocha Msaidizi wa Toto African, Athuman Bilal ‘Bilo’, ameitumia Yanga salamu kwamba lazima itaacha pointi tatu katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, kesho.
“Hii mechi najua itakuwa ngumu lakini sisi tumejiandaa kuhakikisha hatupotezi kwa kuwa tunacheza nyumbani, hivyo ni lazima tushinde tukiwa hapa,” alisema Bilo.
“Tunataka Yanga waache pointi tatu hapa Mwanza, nashukuru kikosi changu kipo fiti, wachezaji wote wapo vizuri,” aliongeza.
Wakati huohuo, Katibu wa Yanga, Lawrance Mwalusako, jana alizungumza na waandishi wa habari na kusema baadhi ya viongozi wa Kamati ya Utendaji watakwenda kuongeza nguvu kwenye mchezo huo wa kesho na kujifunza kwanini timu yao inafungwa ugenini msimu huu.

Comments
Post a Comment