
HALI ya hewa iliyochafuka wakati wa Uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT, imeeleza kuibua vita mpya kati ya mshindi wa kiti hicho, Sophia Simba na aliyemuuliza swali la kichokozi, Shyrose Bhanji.

Shy-Rose Bhanji,
(Kulia), akionyesha uso wa hasira huku akitulizwa na mjumbe mwenzake,
kufuatia tafrani kati yake na mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania
UWT), Sophia Simba.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Shyrose alichukizwa na kitendo cha watu
walioonekana kuwa wafuasi wa Sophia ambao walimzomea kwenye ukumbi wa
mkutano, baada ya yeye kuuliza swali lililotafsiriwa kuwa la kichokozi.“Shyrose amesema watu wa Sophia wamemdhalilisha sana kwa kitendo chao cha kumzomea kiasi cha kutaka kumlazimisha atoke nje, kwa hiyo amesema hakubali na atapambana kwa sababu yeye ni mwanamke jasiri, asiyeogopa chochote,” alisema mtoa habari wetu.
Aliongeza: “Unajua ndani ya CCM kumekuwa na makundi makundi, nadhani Shyrose amesema atapambana kwa kuhisi kwamba Sophia anaweza kutumia nafasi yake ya uenyekiti wa UWT kumbania Shyrose kwenye harakati mbalimbali ndani ya chama.”

Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, swali lililoibua mtafaruku wote ni lile ambalo Shyrose alimtaka Sophia aseme atawasaidiaje wanawake wa CCM kwa sababu tangu amekuwa mwenyekiti wa UWT miaka mitano iliyopita, hakuwahi kuonekana hadharani akifanya kazi za kukisaidia chama hicho.
JIBU LIKAWA HIVI
Chanzo chetu kikasema: “Sophia alijibu kwamba yeye ni mtu wa serikali, kwa hiyo anafanya kazi zake kwa utulivu tena chini kwa chini, siyo mbwatukaji. Akaongeza kwamba Shyrose amepewa ubunge wa Afrika Mashariki juzijuzi, kwa hiyo hawezi kujua kazi zinakwendaje.”

Mbunge
wa bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, (aliyekaa), akitulizwa
hasira na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwkezaji na Uwezeshaji,
Dkt. Mary Nagu, wakati wa kikao cha uchaguzi mkuu wa Jumuiya ya Wanawake
ya CCM, UWT, kwenye ukumbi wa chuo cha Mipango Dodoma Jumamosi Oktoba
20, 2012.
VITA ITAFIKA WAPI?Kwa mujibu wa chanzo chetu, hali ilikuwa mbaya na bila busara za aliyekuwa mwenyekiti wa kikao, Profesa Anna Tibaijuka, ‘wapambe’ wa Sophia wangeweza kumtoa nje Shyrose tena kwa msobemsobe.
Imeelezwa kwamba Tibaijuka alizuia Shyrose kutolewa nje lakini hakuwa na amani baada ya watu hao kuendelea kumzomea.
Jumapili iliyopita, zilifanyika jitihada za kumpata Shyrose hakupatikana lakini Sophia alipopokea simu, alijibu: “Nipo kwenye kikao. Vikao vya chama vinaendelea, nitatoa ufafanuzi baadaye.”
Comments
Post a Comment