
Mchungaji Kiongozi Michael Meela wa Kanisa
la Efatha mkoani Rukwa akiongelea kuhusu suala hilo alisema hasara
iliyopatikana ni zaidi ya shilingi milioni 228 na kwamba tukio hilo
lilitokea mara tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Kwela Mh. Ignas Malocha
kuhutubia mkutano wa hadahara kijijini hapo na kuwahamasisha wananchi
watumie nguvu ya umma kuyakomboa mashamba yao yaliyochukuliwa na
mwekezaji huyo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Bw Jacob
Mwaruanda akithibitisha kuhusu sakata hilo alisema tayari
wanawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kufanya uharibifu huo mkubwa
namsako unaendelea kuwatafuta wengine waliohusika katika tukio hilo.
Comments
Post a Comment