SHABAN KADO AZICHAPA UWANJANI KAMA MWASIKA

http://api.ning.com/files/mHCM4a0eK6sx8g8o13IiXFNIBWDkRs0SyucwL8TTcxWQlotEdXG8ndLxjiu7f0AXUYBccZCy3EsQ0GdECZTb3MTwC0U68SWa/kado.JPG?width=299KIPA wa Mtibwa Sugar, Shaban Hassan ‘Kado’ anaweza kukumbana na adhabu kutoka kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikiwa itabainika kuwa alimpiga shabiki wa Ruvu Shooting, Eddi Masawe ambaye ni askari.
Tukio hilo lilitokea mara baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara baina ya timu hizo Oktoba Mosi ambapo Mtibwa ilishinda kwa mabao 3-2.
Baada ya mchezo huo, Kado alimfuata shabiki huyo na kumpiga ngumi ya mdomo na kumpasua. Mara baada ya kuona hivyo, baadhi ya viongozi wa TFF na wengine kutoka pande zote mbili za klabu, waliingilia na kumtaka Kado aombe msamaha, jambo ambalo alilitekeleza.
Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ameliambia gazeti hili kuwa wao wamemsamehe Kado kwa kuwa wanatambua maana ya soka, lakini wanaiachia TFF iweze kufanya kazi yake kwa kuwa wao walikuwepo uwanjani na walishuhudia tukio hilo.
“Kado alimpiga shabiki wetu Eddi Masawe na kumpasua mdomo, viongozi wa TFF walimtaka aombe radhi na akafanya hivyo,” alisema Masawe.
Kwa mujibu wa kanuni ya 25 ya Ligi Kuu Bara, kifungu cha kwanza G (ii) na (iii), ikiwa itathibitika Kado alifanya kosa hilo, ataadhibiwa kwa kufungiwa michezo isiyopungua mitatu na faini isiyopungua Sh 500,000.

Comments