
WAKATI wasanii ‘classic’ Bongo, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wakiwaomba radhi Watanzania kutokana na kupigwa picha za nusu utupu hivi karibuni, liliibuka sheshe baada ya ‘kutwangwa’ maswali na wanahabari huku Aunt akiangua kilio kwa uchungu, Risasi Mchanganyiko lilikuwepo.
Aunt Ezekiel akiwaomba radhi Watanzania kwa kitendo cha kupigwa picha za nusu uchi stejini.
Matukio hayo yaliyoshuhudiwa na mwandishi wetu, yalijiri Oktoba 15
mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Posta, jijini Dar
wakati wasanii hao walipokuwa wakiomba radhi Watanzania kufuatia matukio
hayo machafu waliyoyafanya hivi karibuni kwenye Tamasha la Fiesta.Aunt ndiye aliyekuwa wa kwanza kufika ukumbini hapo na kuanza kuwaomba radhi Watanzania huku akiahidi kutorudia tena kisha akamuombea udhuru Wema ambaye muda huo alikuwa hajafika.
“Kiukweli familia yangu imeumizwa sana na yale matukio, nimejifunza kuwa makini katika uvaaji wangu na niwaombe Watanzania wanielewe kuwa sitarudia tena,” alisema Aunt huku akiangua kilio.
Baada ya Aunt kuongea hayo, haukupita muda mrefu Wema a.k.a Beautiful Onyinye alifika na kuungana na mwenzake kisha naye kuomba radhi kama alivyofanya mwenzake.

Mrembo Wema Sepetu nae akiwaomba radhi Watanzania.
Alipomaliza, ulifika muda wa waandishi kuuliza maswali ambapo
alipoulizwa kuhusiana na mahojiano aliyofanya mama yake, Mariam Sepetu
kwenye televisheni moja jijini Dar akimsafisha, ghafla Wema aligeuka
mbogo na kuja juu.Mwanadada huyo alianza kubishana na mwandishi huyo aliyeuliza swali akimtaka asiongelee masuala ya familia yake kwani hakuwa pale kwa lengo hilo.
“Anyway basi tufanye yaishe. Niwaombe tu radhi Watanzania na niahidi kwamba hayatajirudia tena na nitakuwa makini zaidi katika uchaguzi wa nguo zangu,” alisema Wema.
Comments
Post a Comment