
Katika uteuzi alioufanya juzi wa
mawaziri, manaibu mawaziri na makatibu wakuu, Dk Shein kwa kutumia uwezo
aliopewa chini ya Kifungu 48(a) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984,
alifuta rasmi uteuzi huo wa Himid.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu
Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Dk Abdulhamid Yahya Mzee
ilieleza kuwa Dk Shein pia amemteua Shawana Bukheti Hassan kuwa Mjumbe
wa Baraza la Mapinduzi kumbadili Mwakilishi huyo wa Kiembesamaki. Uteuzi
huo ulianza juzi.
Hata hivyo, Ikulu ya Zanzibar haikueleza
sababu za kufutwa uteuzi wa Himid ambaye aliomba kujiuzulu pia nafasi
ya Waziri wa Kilimo na Maliasili miezi minne iliyopita.
Katika siku za hivi karibuni, Himid
ambaye ni Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Uchumi na
Fedha Zanzibar, ametangaza rasmi kuwa muumini wa Muungano wa mkataba
ambao unakwenda kinyume cha Sera za chama chake kinachotetea na kulinda
Muungano wa Serikali mbili.
Aidha, Dk Shein kwa kutumia uwezo
aliopewa chini ya Kifungu cha 47 cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984
amefanya uteuzi wa naibu mawaziri kwa kumteua Naibu Waziri wa Kilimo na
Maliasili, Mtumwa Kheir Mbarak na pia Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi
anakuwa Mohammed Said Mohamed.
Katika uteuzi huo, Dk Shein pia ameteua
makatibu wakuu ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano anakuwa Dk Juma Malik Akili wakati aliyekuwa Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Dk Vuai Iddi Lila atapangiwa kazi nyingine.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Makazi,
Maji na Nishati ni Ali Khalil Mirza wakati aliyekuwa Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Mwalim Ali Mwalim atapangiwa kazi nyingine.
Kwa upande wa naibu makatibu wakuu,
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ni Tahir
Abdulla wakati aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Msanif Haji Mussa atapangiwa
kazi nyingine.
Aidha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ardhi, Makazi, Maji na Nishati ni Mustafa Aboud Jumbe ambaye anachukua
nafasi iliyoachwa wazi na Abdulla aliyekwenda Miundombinu na
Mawasiliano. Pia, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi anaeshughulikia Idara Maalumu za SMZ, Julius Nalimy
Maziku anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Juma Abdulla Juma aliyeteuliwa
kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari hivi karibuni.
Pamoja na hao, Naibu Katibu Mkuu wa
Ofisi ya Rais (Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo), Juma Ameir Hafidh
anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Abdi Khamis Faki aliyeteuliwa kuwa
Kamishna wa Bodi ya Mapato (ZRB) hivi karibuni.
Mwingine ni Saleh Ramadhan Ferouz kuwa
Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii anayechukua nafasi iliyoachwa
wazi naMirza aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Makazi,
Maji na Nishati.
Aidha, Mussa Haji Ali ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa
Comments
Post a Comment