
Mchina (jina halikupatikana)amedaiwa kutengeneza mabati feki na kuyagonga nembo ya Shirika la Viwango vya Ubora Tanzania (TBS) katika ghala lililopo Kiwalani Dar, ametiwa mbaroni huku waandishi wa gazeti hili wakishuhudia.
Mbali na Mchina huyo, polisi pia walimtia mbaroni mkalimani wa Mchina huyo aliyefahamika kwa jina la Lyimo na kuwafikisha wote wawili katika Kituo cha Polisi cha Buguruni kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Waandishi wa gazeti hili walikuwepo wakati Mchina na mkalimani wake wakitupwa rumande baada ya kuhojiwa na uchunguzi zaidi wa tukio hilo ukiwa unaendelea wakati ghala la Mchina huyo likiwa limepigwa kufuli.
Kabla ya kumnasa Mchina huyo, polisi walifanya kazi ya ziada kumdhibiti kutokana na kutaka kurusha kareti alipokuwa akigoma kupelekwa kituoni lakini hata hivyo alitulizwa.
Walioshuhudia tukio hilo walilipongeza jeshi la polisi kwa kulishughulikia suala hilo la bidhaa feki na kuitaka serikali kuhakikisha kuwa sheria inachukua mkondo wake.
Tuleteeni mangowela Tumpe dawa
ReplyDelete