POLISI WAKANA KUHUSIKA NA MAUAJI A.KUSINI

Polisi nchini Afrika Kusini, wamekana kuhusika na mauaji ya mwanaume mmoja ambaye mwili wake ulipatikana baada ya makabiliano kati yao na wachimba migodi wakati wa vurugu katika mgodi wa Platinum.

Brigedia mmoja wa polisi, alithibitisha kupatikana kwa mwili huo, ingawa alisema polisi hawakutumia nguvu kupita kiasi katika mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya Anglo American.
Mapema watu walioshuhudia tukio hilo, walisema kuwa polisi waliwapiga risasi wachimba migodi.
Afrika Kusini inakabiliwa na migomo ya wachimba migodi wanaodai nyongeza ya mishahara pamoja na malalamiko chungu nzima ya wafanyakazi wa viwanda vingine katika sekta ya madini.

Comments