NIYONZIMA ANENA YAKE KUHUSU MECHI YAO NA WATANI WAO WA JADI SIMBA

KIUNGO wa kimataifa wa Yanga, Haruna Niyonzima amesema bao la mapema la Simba lililofungwa na Amri Kiemba katika mechi ya Ligi Kuu Bara, juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, ndilo lililowamaliza nguvu.
Niyonzima amesema walicheza kwa nguvu lakini walichokosea ni kuruhusu bao hilo la mapema.
“Bao la Kiemba ndilo lilitufanya tunyong’onyee kwa kuwa lilikuwa la mapema sana, ikabidi tuanze kucheza kwa nguvu ili kulirejesha lakini kama tungeanza sisi, nafikiri isingetusumbua sana.
“Hata hivyo Simba ni timu bora zaidi, ndiyo maana mechi ilikuwa ngumu japokuwa hatukupenda kupata matokeo hayo,” alisema Niyonzima.

Comments