Mwili
wa mwanafunzi wa darasa la tatu, Shule ya Msingi Iwambi, Jijini Mbeya,
Kelvin Patrick (8) ukiwa umefunikwa baada ya kufariki dunia kutokana na
kujinyonga kwa kutumia kamba ya viatu katika bomba la maji nje ya nyumba
yao.
Baadhi ya majirani waliojitokeza kushuhudia mwili wa mwanafunzi wa darasa la…
Mwili
wa mwanafunzi wa darasa la tatu, Shule ya Msingi Iwambi, Jijini Mbeya,
Kelvin Patrick (8) ukiwa umefunikwa baada ya kufariki dunia kutokana na
kujinyonga kwa kutumia kamba ya viatu katika bomba la maji nje ya nyumba
yao.
Baadhi
ya majirani waliojitokeza kushuhudia mwili wa mwanafunzi wa darasa la
tatu, Shule ya Msingi Iwambi, Jijini Mbeya Kelvin Patrick (8.
Mama
mzazi wa marehemu Kelvin Patrick (8), Bi Subira Patrick (38) akiwa
katika hali ya majonzi kufuatia kifo cha mwanae aliyejinyonga.
(Picha na Ezekiel Kamanga / Mbeya Yetu Blog)
-----
(Picha na Ezekiel Kamanga / Mbeya Yetu Blog)
-----
Mwanafunzi
wa Shule ya Msingi Iwambi, darasa la tatu Kelvin Patrick (8) jinsia ya
kiume amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya viatu
katika bomba ya maji nje ya nyumba yao.
Tukio hilo limetokea Oktoba 27 mwaka huu
majira ya saa 5 kamili usiku wakati wazazi wote wa mtoto huyo Bwna
Patrick Mwakapalila(52) na Bi Subira Patrick(30) wakiwa hawapo nyumbani
na kwamba baba mzazi akiwa na mwanae wa kiume aitwaye Joshua Patrick(10)
waliondoka majira ya saa 3:30 kuelekea mjini.
Aidha Baba wa mtoto huyo alipigiwa simu
na mtu mmoja kwamba arejee nyumbani na yeye pasipo kuchelewa alirejea na
kumkuta mwanae amejinyonga katika bomba la maji kwa kutumia kamba ya
viatu na chini kukiwa na ndoo, ambapo kifo hicho kimezua maswali mengi
kwani kimo cha mtoto ni zaidi ya futi mbili na nusu na urefu wa kamba
hali inayotia shaka kuwa mtoto huyo alichukua uamuzi huo yeye mwenyewe.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Ivwanga, Bwna
Chonde Kalisto amethibitisha tukio hilo la kusikitisha na kwamba yeye
alipokea taarifa kutoka kwa Balozi wake Bi Esther Mahenge ambapo walitoa
taarifa polisi ambapo walifika eneo la tukio kisha kuuchukua mwili wa
marehemu kwa uchunguzi zaidi na hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa
kuhusiana na tukio hilo.
Comments
Post a Comment