KOCHA MPYA YANGA AANZA KAZI YA KUKINOA KIKOSI ILI KUMKABILI MNYAMA










Kocha mpya wa mabingwa wa kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati mholanzi Ernstus
Wilhelmus Johannes Brandts ameanza kazi rasmi kukinoa kikosi cha Yanga leo asubuhi katika uwanja wa shule ya Sekondari Loyola tayari kwa ajili ya kumkabili Mnyama siku ya jumatano.
Emstus ataiongoza Yanga katika mchezo wa watani wa jadi utakaofanyika siku ya jumatano uwanja wa Taifa na kuonyeshwa moja kwa moja ni kituo cha runinga cha supersport cha nchini Afrika Kusini kuanzia majira ya saa 1 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Yanga imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kocha Emstus kwa ajili ya kuifundisha, ambapo katika benchi lake atashirikiana na kocha mzawa Fred Felix Minziro na kocha wa makipa Mfaume Athumani.
Akizungumzia kikosi cha Yanga kocha Brandts amesema amefurahi kuifundisha Yanga, timu kubwa yenye mashabiki wengi ukanda wa wa Afrika Mashariki, ana imani kuwa timu yake itainuka na ushindi katika mchezo huo.
Yanga naifahamu vizuri hata kuja kuifundisha, kwani nilishacheza nayo nikiwa na APR kwa katika miaka miwli, hivyo wachezaji wake nawatambua vizuri na timu tunayocheza nayo siku ya jumatano Simba sc naifahamu pia kwani niliwaona pia katika mashindano ya kagame alisema 'Brandts'
Aidha aliongeza kuwa 'Nitaingia uwanjani kwa lengo moja tu la kusaka point 3 muhimu ili kusogea katika nafasi ya kuweza kuongoza ligi na kuelekea kutwa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom 2012/2013.'

Comments