Nawashukuru baada ya
kunitaka niwape muda wa kulitafakari walinikubalia lakini wakaniomba
nibakie hadi tutakapokamilisha baadhi ya shughuli muhimu za Chama katika
kipindi hichi. “Sababu kubwa zilizonisukuma kukiomba Chama kiniruhusu
niachie nafasi hii ni kutokana na muda mrefu sasa kuhisi kwamba majukumu
niliyo nayo ya kuwa msimamizi mkuu wa utendaji wa Chama kwa upande wa
Zanzibar na wakati huo huo kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa jimbo
la Mji Mkongwe hakunipi fursa ya kujifaragua na kutumikia nafasi zote
mbili kwa ufanisi unaotakiwa.
Nataka kuona kazi ya
kuibana Serikali ndani na nje ya Baraza ili iwajibike zaidi kwa wananchi
inaimarika zaidi. “Sambamba na sababu hiyo ni kwamba nimekusudia
kutumia muda mwingi zaidi kutoa mchango mkubwa zaidi katika harakati za
wananchi wa Zanzibar zinazoendelea za kuhakikisha kuwa Zanzibar
inarejesha mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na
kuwepo kwa Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika yenye mamlaka
kamili kitaifa na kimataifa. “Harakati zinazoendelea Zanzibar kwa njia
za amani na za kidemokrasia kwa kutumia mchakato wa Katiba Mpya
zinahitaji kuungwa mkono na kupewa msukumo wa dhati na Wajumbe wa Baraza
la Wawakilishi waliochaguliwa na wananchi wa Zanzibar kwenda kusimamia
maslahi yao na ya nchi yao.
Nimetafakari na kuona
kwamba nikiwa sina majukumu mengine ya kiutendaji nitakuwa na muda
kutosha wa kulifanya hili mimi na Wawakilishi wenzangu tunaotoka CUF na
CCM, vyama viwili vya siasa vilivyomo Barazani. “Nafurahi kwamba leo
nimetimiza azma yangu hiyo. Pamoja na uamuzi huu, naendelea kubaki kuwa
Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa
Taifa. “Nawahakikishia viongozi na wanachama wenzangu wa CUF kwamba
tutaendelea kushirikiana pamoja katika shughuli nyengine zote za kisiasa
za Chama na kwa pamoja tutafanya kazi kuyatimiza malengo tuliyojiwekea.
Naahidi kumpa ushirikiano kikamilifu mwanachama yeyote atakayeteuliwa
kujaza nafasi ninayoiwacha.
” HAKI SAWA KWA WOTE ”
ISMAIL JUSSA
http://www.hakingowi.com/
OK Mr Alvaro i will do that.
ReplyDelete