
ULE wakati wa kimbembe cha huko Spain kinachofuatiliwa Duniani nzima, maarufu kama El Clasico, umefika na leo Usiku Saa 2 Dakika 50 Usiku, Saa za Bongo, Uwanja wa Nou Camp utawaka moto pale vinara wa La Liga Barcelona watakapocheza na Mahasimu wao Real Madrid ambao ndio Mabingwa watetezi katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi.
Barcelona ndio wanaongoza La Liga hadi sasa wakiwa Pointi 8 mbele ya Real Madrid ambao wako nafasi ya 6.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO TIMU za JUU:
1 Barcelona Mechi 6 Pointi 18
2 Atletico Madrid Mechi 6 Pointi 16
3 Malaga Mechi 6 Pointi 14
4 Real Betis Mechi 7 Pointi 12
5 Real Mallorca Mechi 6 Pointi 11
6 Real Madrid Mechi 6 Pointi 10
7 Real Valadoid Mechi 7 Pointi 10
+++++++++++++++++++++++
HALI za KILA TIMU:
FC Barcelona
Barcelona wataingia kwenye Mechi ya leo
bila ya Kepteni wao Carles Puyol na pengine bila ya Sentahafu wao
mwingine Pique ambae alikuwa akiuguza mguu wake.
Mapengo hayo huenda yakamlazimisha Kocha
wa Barca Tito Vilanova kuwachezesha Viungo Alex Song na Mascherano kama
Masentahafu huku Jord Alba na Alves wakicheza kama Mafulbeki.
Kwenye Kiungo ndiko injini ya Barca na, bila shaka, watakuwepo Xavi, Busquets na Iniesta.
Mbele Supastaa Lionel Messi anaweza
kushirikiana na Pedro huku David Villa akitinga dimbani baadae kwenye
Mechi pamoja na Chipukizi Tello.
Kikosi kinaweza kuwa [Mfumo 4-3-3]: Valdes; Alves, Mascherano, Song, Alba; Xavi, Busquets, Cesc; Messi, Pedro, Tello.
Real Madrid
Kwa Mameneja wangu kuwa Pointi 8 nyuma
ya Timu ambayo inasifika ni bora Duniani kunaweza kuwatia mchecheto
lakini si kwa Jose Mourinho ambae hujisifia wenyewe kuwa ni ‘Mtu
Spesheli’ na sasa akijiita ‘Mtu pekee.’
Kikosi cha Real ni imara na kimesheheni Wachezaji mahiri kuanzia Kipa Iker Casillas hadi mbele kwa Supastaa Cristiano Ronaldo.
Upo kila uwezekano Difensi yao ikawa na Arbeloa, upande wa kulia, Masentahafu Pepe na Ramos na Beki wa kushoto ni Marcelo.
Kwenye Kiungo, Jose Mourinho ana
Wachezaji kibao wa kuwachagua na upo uwezekano Ricardo Izecson dos
Santos Leite, maarufu kama Kaka, akapata muda wa kuonekana Uwanjani
baada ya kuonyesha cheche zake kwa mara nyingine tena hivi karibuni.
Viungo wengine wanaoweza kuwepo ni kati ya Alonso, Khedira, Ozil, Di Maria, Essien na Modric.
Kikosi kinaweza kuwa [Mfumo 4-2-3-1]: Casillas; Arbeloa, Ramos, Pepe, Coentrao; Alonso, Khedira; Ozil, Di Maria, Ronaldo; Benzema
Comments
Post a Comment