HIVI NDIVYO KAMANDA LIBERATUS BARLOW ALIVYOAGWA KWA MAJONZI MAKUBWA

MWILI wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow leo umeagwa katika Kanisa la Mtakatifu Augustino lililopo Ukonga jijini Dar es Salaam. …

MWILI wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow leo umeagwa katika Kanisa la Mtakatifu Augustino
lililopo Ukonga jijini Dar es Salaam.
 
Mwili wa marehemu, Kamanda Liberatus Barlow ukiingizwa nyumbani kwake Ukonga eneo la Sabasaba jijini Dar leo.
Kamanda Barlow aliuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia Jumamosi na watu wanaodaiwa kuwa majambazi katika eneo la Kitangiri jijini Mwanza. Mwili wa Kamanda Barlow umeagwa kwa heshima zote na viongozi mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi na unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda Moshi kwa ajali ya mazishi.
PATA PICHA ZA TUKIO HILO HAPA:
Maofisa wa Polisi wakijiandaa kushusha mwili wa marehemu, Kamanda Barlow kanisani.
Aliyewahi kuwa IGP, Omar Mahita akielekea kanisani kwa ajili ya ibada ya kuuaga mwili wa Barlow.
 
IGP Said Mwema (katikati) akiwasili eneo la kanisa tayari kwa ibada ya kuuaga mwili wa Kamanda Barlow.
 
Askari wakipokea jeneza lenye mwili wa Kamanda Barlow kuelekea kanisani.
 
Padri Steven Nyilawila aliyeongoza ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Barlow katika Kanisa la Mt. Augustino -  Ukonga jijini Dar leo.
 
IGP Said Mwema (kushoto), Omar Mahita (kulia) pamoja na maofisa wengine wa Jeshi la Polisi wakiwa kanisani.
 
Wanakwaya wa Kanisa la Mt. Augustino Ukonga wakiimba wakati wa ibada.
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye (kulia) akiwa na Mstahiki Meya wa Manisapaa ya Ilala, Jerry Slaa kanisani.
(PICHA ZOTE NAGPL)

Comments