
Chanzo chetu kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, tukio hilo lilijiri hivi karibuni usiku wa manane baada ya Dallas kufika nyumbani kwa msanii huyo maeneo ya Mwananyamala jijini Dar na kugonga mlango kwa fujo akitaka afunguliwe.
“Aligonga sana kiasi cha kuwa kero kwa majirani, alipoona hafunguliwi akenda kugonga dirishani. Mdogo wa Snura akaamka na kumuuliza anataka nini ndipo akasema anamtaka Snura ili aondoke naye.
“Mdogo mtu akamwambia amelala na amechoka hawezi kutoka, baada ya Dallas kujibiwa hivyo hakuridhika, akaendelea kugonga na alipoona kimya akaondoka,” kilidai chanzo hicho.
Katika kupata undani wa tukio hilo, mwandishi wetu alimtafuta Dallas bila mafanikio lakini Snura alipopatikana alikiri kuletewa fujo hizo na mshikaji huyo.
“Ni kweli tukio hilo lilitokea na baada ya kugonga sana, mimi sikutoka hivyo akaondoka zake, sijui alitaka anipeleke wapi usiku huo,” alisema Snura.
Comments
Post a Comment