CRISTIANO RONALDO ATUMA SALAMU KWA BARCA

Real Madrid watajikita kwenye EL Clasico ya La Liga huko Nou Camp kucheza na Barcelona Wikiendi ijayo wakiwa Pointi 8 nyuma ya
Mahasimu wao hao lakini, bila shaka, ‘salamu spesho’ toka kwa Cristiano Ronaldo zimeshafika huko Nou Camp baada ya jana Supastaa huyo kuitoa Real nyuma kwa Bao moja na kupiga hetitriki iliyoiwezesha Real kuikung’uta Deportivo La Coruna bao 5-1.
Real, wakitawala, walijikuta wako nyuma katika Dakika ya 16 baada ya Riki kuifungia Deportivo bao.
Lakini Real walizinduka na kupiga bao 3 kabla Haftaimu kwa bao za Ronaldo. Bao mbili, na Di Maria.
Kipindi cha Pili Ronaldo aliongeza moja na Pepe kupiga jingine.
Ushindi huo umewafanya Real wachupe hadi nafasi ya 6 wakiwa na Pointi 10 kwa Mechi 6.
Serie A
Edinson Cavani, baada ya kupiga hetriki hapo Jumatano dhidi ya Lazio, jana alifunga Penati ya Kipindi cha Pili na kuipa Napoli ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Sampdoria na kuifuta rekodi ya Timu hiyo ya kutofungwa Msimu huu.
Ushindi huu wa Napoli umewafanya wafungane Pointi na Mabingwa Juventus, ambao Jumamosiwaliwatandika AS Roma 4-1, wote wakiwa na Pointi 16 kila mmoja toka Mechi 6.
Kwenye Mechi hiyo na Sampdoria, Kocha wa Napoli Walter Mazzari alitolewa nje katika Kipindi cha Kwanza kwa Kadi Nyekundu baada ya kulalamika kwa nini Pedro Obiang hakutolewa nje kwa Rafu mbaya aliyomfanyia Pablo Cannovaro.

Comments