CHAZ BABA: KUTANGAZA NDOA NA LULU KUMENILETEA BALAA


RAIS wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ yupo kwenye gogoro zito na wanawake aliozaa nao, mama Jack na mama Carina baada ya hivi karibuni kutangaza ndoa na staa wa filamu aliye gerezani, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na habari hiyo kuandikwa kwenye gazeti hili.

 
Elizabeth Michael ‘Lulu’
Akipashana na Motomoto Newz juzikati, Kijitonyama, Dar,  Chaz Baba alisema katika stori za magazetini kwa mwaka huu, ya kumuoa Lulu imemfikisha pabaya.
“Ilipotoka tu ile habari, wakanipigia simu kila mmoja kwa wakati wake, maswali mengi, nilijaribu kuwaweka sawa lakini hakuna aliyenisikiliza zaidi ya kunikatia simu,” alisema Chaz Baba.

Comments