BAHANUZI AMPA PROGRAMU KABAMBE SHOMARI KAPOMBE

BEKI kinda wa Simba, Shomari Kapombe, Ijumaa iliyopita alishindwa kufanya mazoezi ya nguvu na wenzake kutokana na kifundo chake cha mguu kutokuwa sawa.
Kapombe alionekana kukimbia muda wote huku mabeki wenzake wakijifunza kuzuia mashuti yaliyokuwa yakipigwa na washambuliaji.
Katika mazoezi hayo yaliyoanza saa 10 jioni, wachezaji wote walianza kwa kupasha misuli kisha wakajifunza kupiga mashuti, penalti na kuzuia mashuti. Muda wote huo Kapombe alikuwa akikimbia tu na kuuzunguka Uwanja wa Kinesi, Dar, zaidi ya mara tano.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Kapombe alisema kifundo cha mguu alichoumizwa na Said Bahanuzi bado kinamsumbua.
“Yah! Enka inanisumbua lakini mimi nachukulia kama sehemu ya mchezo kwa kuwa najua Bahanuzi alikuwa timu pinzani, hivyo ilikuwa lazima aitetee timu yake,” alisema Kapombe.
Kwa upande wa Daktari wa Simba, Cosmas Kapinga alisema Kapombe yupo fiti japokuwa alikuwa na maumivu.

Comments