Chuji ambaye alikuwa akishirikiana na Haruna Niyonzima katika mechi hiyo, alipiga pasi 49 ambapo 35 ziliwafikia walengwa.
Niyonzima, raia wa Rwanda, ndiye aliyefuatia kwa kupiga pasi 33 huku 26 zikifika zilikotakiwa kufika.
Mwinyi Kazimoto wa Simba licha ya kutolewa nje katika kipindi cha pili kutokana na majeraha, alipiga pasi 30 huku mbili zikishindwa kufika kwa walengwa, kizuri zaidi pasi yake ya tatu ndiyo iliyozaa bao la Simba.
Kiungo kinda wa Simba, Jonas Mkude alipiga pasi 31 katika kipindi chote alichokuwepo dimbani kabla ya kutoka katika dakika ya 68 na nafasi yake kuchukuliwa na Haruna Moshi ‘Boban’. Mkude alikosea pasi nne na kufikisha 27.
Frank Domayo (Yanga) na Amri Kiemba (Simba), walijitengenezea sifa za kipekee, kwani licha ya kupiga pasi chache, walifanya kazi kubwa ya kutengeneza mashambulizi na kusababisha kashikashi katika lango la wapinzani.
Comments
Post a Comment