ALIYEDAIWA KUFA KISA BAO LA SIMBA, AZIKWA KWA MAJONZI

YULE mzee Urban Ndugulu anayedaiwa kukutwa na mauti baada ya mchezaji wa Simba, Amri Kiemba kupachika bao la kwanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar Jumatano iliyopita, hatimaye amezikwa kwa majonzi.
Mwanahabari wetu ambaye alikuwa shuhuda wa tukio hilo lililotokea kwenye Viwanja vya Mashujaa mjini hapa, aliungana na umati uliofurika ukiongozwa na mashabiki wa Yanga katika kumsindikiza mzee Ndugulu katika nyumba yake ya milele.
Mke wa mzee huyo, Veronica Ndugulu alishindwa kujizuia kwa kuishiwa nguvu wakati wa kuuaga mwili wa mumewe nyumbani kwake maeneo ya Mafiga na kusababisha majozi maradufu kwa waombolezaji hadi mwisho wa maziko hayo.

Comments