
>>NUSU FAINALI: Mazembe v Esperance, Al
Ahly v Sunshine Stars!
LEO, kwenye Mechi za Kundi B, Bechem Chelsea ya Ghana iliichapa TP Mazembe kwa bao 1-0 na Al Ahly kutoka sare ya 1-1 na wenzao wa Misri Al Zamalek na hivyo kufanya Nusu Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI kuwa ni Mechi kati ya Esperance ya Tunisia, ambao ni Mabingwa watetezi, kucheza na TP Mazembe na Al Ahly kuivaa Sunshine Stars ya Nigeria.
Kabla ya Mechi za leo, ilikuwa tayari inajulikana Timu zipi zipo Nusu Fainali lakini kilichongojewa ni kujulikana nani atamaliza juu toka Kundi B ili kujua Esperance, aliemaliza Mshindi Kundi A, atacheza na nani na Sunshine Stars atapambana na nani.
Mechi za Nusu Fainali zitachezwa Mwezi ujao Oktoba kwa Mechi ya kwanza Oktoba 6 na marudiano Oktoba 20.
================
MSIMAMO=CHAMPIONZ LIGI:
KUNDI A
1 Esperance Mechi 4 Pointi 9==Imeingia Nusu Fainali
2 Sunshine Stars Mechi 4 Pointi 6==Imeingia Nusu Fainali
3 ASO Chlef Mechi 4 Pointi 3
FAHAMU: ES Sahel ya Tunisia imeondolewa kwenye Mashindano na CAF
KUNDI B
1 Al Ahly Pointi Mechi 6 Pointi 11 [Magoli 9 kwa 6] ==Imeingia Nusu Fainali
2 TP Mazembe Mechi 6 Pointi 10 [Magoli 9 kwa 6] ==Imeingia Nusu Fainali
3 Bechem Chelsea Mechi 6 Ponti 9
4 Al Zamalek Mechi 6 Pointi 2
Comments
Post a Comment