YANGA: YONDANI NI WETU 100%


Uongozi wa klabu Yanga umesema suala la pingamizi la wachezaji Kelvin Yondan na Mbuyi Twite linazungumzwa kishabiki bila kuangalia ukweli wa jambo husika na kusisitiza hakuna makubaliano ya kukutana na uongozi wa Simba ili kumalizana.


Aidha, Yanga imewataka mashabiki wa klabu hiyo kuondoa hofu kwa kuwa wachezaji hao si mali yao.

Akizungumza na NIPASHE jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Selestine Mwesigwe alisema hakuna barua iliyofika ofisini kwake ya kuombwa kukutana na Simba na kusisitiza kuwa kamati ya shirikisho la soka, TFF, ya Alex Mgongolwa iachwe ifanye kazi yake.

"Mashabiki na Wanachama wetu wamekuwa na hofu ya kuwapoteza wachezaji hawa... lakini uongozi hauna shaka na jambo hili," alisema.

"Hawa (wachezaji) ni mali yetu ila kwa sasa ngoja tuiache kamati ya (ya TFF ya Haki, Maadili na Hadhi ya Wachezaji chini ya Alex) Mgongolwa ifanye kazi yake."

Mwesigwe alisema uongozi wa klabu hiyo umeachana na sakata hilo na upo katika maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kwa ligi kuu ya Bara.

Alisema Yanga haitaki kujichanganya na mambo mengine na badala yake wapo makini na maandalizi ya kikosi chao kabla ya kuanza kwa ligi.

"Tunaamini tulichokifanya na tunaamini kamati hii ya Mgongolwa na wajumbe wake watafanya kazi yao kwa kufuata kanuni na sheria zilizopo na mwisho wa siku tutasimama kwenye haki... hatuna hofu na hili," alisema Mwesigwe.

Katika hatua nyingine, Mwesigwe amwataka wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuipa sapoti timu hiyo katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu wa ugenini dhidi ya Prisons utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Alisema kuwa wasiwe na hofu na kikosi hicho kwa kuwa kocha wao Tom Saintifiet amewahakikishia timu iko tayari kwa ligi kuu.

Alisema kuwa hawatgemei kucheza mchezo mwingine wa kirafiki kwa kuwa kocha Saintfiet anataka kumaliza programu yake kabla ya kuanza kwa ligi hiyo.

Comments