Skip to main content
WAZIRI PINDA AWAVUA MADARAKA WAKURUGENZI SITA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
amewavua madaraka wakurugenzi sita na kuwateua Kaimu Wakurugenzi sita,
wakurugenzi wapya 14 na kuwahamisha 27 kutoka katika vituo vyao
Miongoni mwa sababu hizo ni pamoja
na kuonyesha udhaifu katika kutekeleza majukumu, kustaafu, kujaza nafasi
zilizo wazi katika Halmashauri mpya zilizoanzishwa hivi karibuni na
wengine kubadilishiwa majukumu na kurejeshwa katika kazi zao za awali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa, Hawa Ghasia akitangaza Wakurugenzi hao na maeneno waliyotoka
kwenye mabano ni Willy Njau (DC Mwanga ) aliomba kurejeshwa katika
majukumu yake ya awali kutokana na sababu za kiafya, Mpangalukela Tatala
(DC Geita), kushindwa kusimamia rasilimaliwatu na fedha, Theonest
Nyamhanga (DC Kishapu), kushindwa kusimamia rasilimaliwatu na fedha.
Wengine ni Eden Munisi (DC Morogoro), kuisababishia Halmashauri kupata
hati chafu na kushindwa kusimamia rasilimali pamoja na uzembe, Mhando
Senyagwa (DC Kyela), kuwa na kesi mahakamani, Nicholaus Kileka (DC
Ngorogoro), alikuwa na kesi inayoendeshwa na Taasisi ya Kudhibiti na
Kupambana Rushwa (Takukuru).
Wakurugenzi wapya walioteuliwa kujaza nafasi zilizo wazi ni Abdallah
Kindwanka, aliyekuwa Afisa Ardhi na Wilaya ya Mufindi ambaye
amehamishiwa Geita kama Kaimu.
Wengine ni Ritius Bilakwata aliyekuwa Mkurugenzi Wilaya ya Kishapu,
kuteuliwa kama Kaimu wilaya hiyo, aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya
Mpanda, Naomi Nko amehamishiwa Wilaya ya Magu, aliyekuwa Mkurugenzi
Wilaya ya Ukerewe, Abdallah Mfaume, amehamishiwa Kyela kushika nafasi
hiyo.
Aidha aliyekuwa Mkurugenzi Wilaya ya Monduli, Twalib Mbasha, ameteuliwa
kukaimu nafasi hiyo wilaya hiyo, aliyekuwa Mkurugenzi Wilaya ya Urambo,
Henry Ruyagu, ameteuliwa kukaimu nafasi hiyo wilaya hiyo na Adam Mgowi,
aliyekuwa Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali amekuwa Mkurugenzi wa
Wilaya ya Mbarali.
Wengine ni Estomih Chang’a aliyekuwa Manispaa ya Arusha na Kaimu
Mkurugezi wa Wilaya amepelekwa Wilaya ya Mpanda kuwa Mkurugenzi,
aliyekuwa Mkurugenzi wa Kibaha, Leti Shuma amehamishiwa Wilaya ya Mwanga
kwa nafasi hiyo na aliyekuwa Mkurugenzi wa Kilosa, Mohamed Maje
amepelekwa Wilaya ya Namtumbo kwa nafasi hiyo.
Fulgency Mponji aliyekuwa Afisa Wilaya wa Manispaa ya Songea amepelekwa
Moshi kuwa Mkurugenzi, aliyekuwa Mkurugenzi wa Njombe, Robert Nehata
amehamishiwa Wilaya ya Tunduru kwa nafasi hiyo, Isabela Chilumba
amekuwa Mkurugenzi Wilaya ya Kahama.
Aidha, aliyekuwa Mkurugenzi wa Kilombero, Fikiri Malembeka amepelekwa
Wilaya ya Sengerema kwa nafasi hiyo, aliyekuwa Mkurugenzi wa Tandahimba,
Isabela Chiluba amepelekwa Wilaya ya Ulanga kwa nafasi hiyo na
aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Mufindi, Nasib Mbaga, amehamishiwa
Biharamulo kwa nafasi hiyo.
Aliyekuwa Mkurugenzi Wilaya ya Nzega, Idd Nganya, amepelekwa Makete kwa
nafasi hiyo, Jovin Jungu, aliyekuwa TC Masasi amepelekwa Wilaya ya
Chamwino kuwa Mkurugenzi, aliyekuwa Manispaa Iringa, Paul Malala
amepelekwa Wilaya ya Njombe kuwa Mkurugenzi na aliyekuwa Mkurugenzi wa
Wilaya ya Bukoba, Felix Mabada, amepelekwa Hanang kwa nafasi hiyo hiyo.
Wakurugenzi waliohamishwa ili kujaza vituo wazi ni pamoja na aliyekuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kilindi, Bibie Mnyamagola amepelekwa
Kongwa kwa nafasi hiyo, Daudi Mayeji aliyekuwa Mkurugenzi Wilaya ya
Chamwino amepelekwa Kilindi kwa nafasi hiyo hiyo.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Igunga, Protace Magayane, amepelekwa
Wilaya ya Nkasi na aliyekuwa Nkasi, Saada Mwaruka amehamishiwa Wilaya ya
Mkuranga.
Aidha, Sipora Liana aliyekuwa Mkurugenzi Wilaya ya Mkuranga amepelekwa
Tabora na aliyekuwa Tabora, Hadija Makuwani ameteuliwa kuwa Mkurugenzi
Wilaya ya Tabora.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya Tabora, Doroth Rwiza amepelekwa Wilaya
ya Kasulu kwa nafasi hiyo na aliyekuwa Mkurugenzi wa Kasulu, Kelvin
Makonda, amepelekwa Wilaya ya Lindi kwa nafasi hiyo hiyo.
Mkurugenzi wa wa Wilaya ya Ulanga, Pudenciana Kisaka amepelekwa Wilaya
ya Iringa , aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Iringa, Tina Sekambo
amepelekwa Makambako.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Bukoba Beatrice Dominic amepelekwa
Wilaya ya Masasi kwa nafasi hiyo, Gladyness Ndyamvuye aliyekuwa
Mkurugenzi Wilaya ya Masasi amepelekwa Wilaya ya Bukoba.
Mkurungenzi wa Wilaya ya Musoma, Nathan Mshana, amepelekwa Wilaya ya
Ngorongoro kwa nafasi hiyo, Mkurugenzi wa Wilaya ya Magu, Cornel
Ngundungi, amepelekwa Wilaya ya Ngara kwa nafasi hiyo.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Njombe, Mohamed Mkupete amepelekwa Manispaa ya
Mtwara, Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro, Dk Koroine Ole Kuney
amepelekwa Wilaya ya Misungwi na Mkurugenzi wa Wilaya ya Tunduru,
Ephraem Ole Nguyaine amepelekwa Wilaya ya Rorya.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Hanang, Goody Pamba amepelekwa Wilaya
ya Igunga kwa nafasi hiyo, Mkurugenzi wa Wilaya ya Tarime, Fidelis
Lumato, amepelekwa Wilaya ya Ludewa.
Aidha, Mkurugenzi wa Wilaya ya Kongwa, Athmani Akalama amehamishiwa
Wilaya ya Tarime na Mkurugenzi wa Mji wa Lindi, Ahmad Sawa amepelekwa
Halmashauri ya Musoma.
Wakurugenzi waliohamishwa kwenda kwenye Halmashauri Mpya ni aliyekuwa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara, Magreth Nakainga amepelekwa Geita,
Mkurugenzi wa Wilaya ya Wilaya ya Kahama, Eliza Bwana amepelekwa
Bariadi.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Biharamulo, Zuberi Mbyana amepelekwa Ilemela,
Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga, Mohamed Nanyanje amepeleka Masasi,
Mkurugenzi wa Wilaya ya Sengerema, Erica Musika amepelekwa Kahama na
Mkurugenzi wa Wilaya ya Makete, Imelda Ishuza amepelekwa Wilaya ya
Busokelo.
Hata hivyo Waziri Ghasia alisema Serikali haitasita kuchukua hatua pale
inapobidi ili kuboresha utendaji kazi na kuwafanya watumishi wawajibike
katika majukumu yao ipasavyo.
Comments
Post a Comment