Skip to main content
WAANDISHI WA HABARI WABUGHUDHIWA NCHINI MADAGASCAR
Jumuia ya waandishi wa habari wa
Madagascar inasema kuwa wanachama wake wanazidi kubughudhiwa na wakuu
wa serikali na baadhi ya wananchi pia.
Jumuia hiyo, Association des Journalistes de
la Presse Privee de Madagascar, imesema inawaunga mkono waandishi wa
habari watatu ambao wamepewa hifadhi kwenye ubalozi wa Afrika Kusini
nchini Madagascar.
Ubalozi ulithibitisha siku ya Ijumaa kuwa,
watu hao watatu, ambao walikuwa wakifanya kazi katika kituo cha redio
cha upinzani ambacho sasa kimefungwa, walipewa hifadhi mwezi uliopita.
Jumuia imesema waandishi hao wa habari wamekuwa wakibughudhiwa kwa muda mrefu.
Comments
Post a Comment