
Habari kutoka kwa chanzo chetu makini ambacho ni ndugu wa karibu na familia hiyo, kwa sharti la kutotajwa gazetini alisema, afya yake bado haijaimarika tangu aliporejea kutoka nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Appolo.
CHANZO KINATIRIRIKA
“Hili suala ni la kifamilia zaidi na linafanyika kwa siri sana, kwahiyo usinitaje mahali popote...kiukweli hali ya Vengu bado hairidhishi. Tangu amefika tumejitahidi sana kumfanyisha mazoezi kama tulivyoelekezwa na madaktari wake lakini wapi!
Katika hatua nyingine, memba wa Kundi la Orijino Komedi aliye Mkurugenzi wa wasanii hao, Isaya Mwakilasa ‘Wakuvywanga,’ alithibitisha kuwa Vengu bado ni mgonjwa.
“Sizungumzi kama Mkurugenzi wa Orijino Komedi lakini ukweli, jamaa bado anaumwa, nadhani juhudi za kumpatia tiba zaidi zinapaswa kufanyika mara moja,” alisema Wakuvanga.
Comments
Post a Comment