Kama kawaida, Barcelona na Real Madrid, ndio walikuwa wanunuzi wakubwa.
Barcelona ndio walioingia sokoni mapema
na kumnunua Jordi Alba kutoka Valencia kwa Pauni Milioni 11.2 kwa vile
walijua Beki wao Eric Abidal ni mgonjwa na nafasi yake inabidi kuzibwa.
Pia, Barcelona walitambua kuwa kuondoka kwa Seydou Keita kwenda China
kumeweka pengo la Kiungo Mkabaji ambae pia anaweza kucheza Sentahafu
kama vile alivyokuwa akiwafanyia Yaya Toure na ndio maana wakalazimika
kumnunua Alex Song kutoka Arsenal kwa Pauni Milioni 15.
Ibrahim Afellay aliondoka Barca kwenda
Schalke kwa mkopo ili kutoa nafasi kwa Vijana Cristian Tello, Isaac
Cuenca na Gerard Deulofeu kupata namba na pia kurudi tena dimbani kwa
David Villa baada ya kupona mguu.
Mahasimu wa Barca, Real Madrid, wao
walikuwa kwenye vuta nikute na Tottenham lakini mwishowe wakampata
Kiungo Luka Modric kwa Dau la Pauni Milioni 33 na pia kumchukua Michael
Essien kwa mkopo kutoka Chelsea.
Uhamisho mwingine uliotokea huko Spain
ni ule wa Athletic Bilbao kumuuza Javi Martinez kwa Bayern Munich kwa
Pauni Milioni 30, kutua kwa Emre Belozoglu huko Atlético Madrid,
Theofanis Gekas kwenda Levante na Simão Sabrosa kwenda Espanyol.
Pia mikopo ya Wachezaji wa Arsenal Joel Campbell kwenda Real Betis na Park Chu-young kwenda Celta Vigo.
Baada ya kumuuza Jordi Alba huko Barca, Valencia walilazimika kumnunua Aly Cissokho wa Lyson ili kuziba pengo.
Italy
Timu kubwa huko Italy zilichangamka
sokoni lakini hakuna hata moja iliyolipa Ada kubwa ya kupindukia na kwa
mara nyingine tena, Juventus na Inter Milan, ndizo ziliizidi AC Milan
kwa uchangamfu wa sokoni.
Juventus walimchukua Nicklas Bendtner
kwa mkopo kutoka Arsenal baada ya kumkosa Dimitar Berbatov, pamoja na
kuwachota Sebastian Giovinco, Lúcio, alieachwa na Inter Milan, na
Rubinho kama Kipa wa akiba.
Inter Milan wao waliwanasa Antonio
Cassano toka AC Milan, Walter Gargano kutoka Napoli na Kipa wa Slovakia
Samir Handanovic toka Udinese ili kumbadili Júlio César aliehamia Queens
Park Rangers.
Maicon pia aliihama Inter Mila kwenda Manchester City kwa Dau la £3m.
AC Milan wao walimnasa Giampaolo Pazzini
kwa kumbadili na Cassano, na ingawa waliwapoteza Mastaa wao Thiago
Silva na Zlatan Ibrahimovic kwa Paris Saint-Germain, kutua kwa Bojan
Krkic kwa mkopo, Cristian Zapata na Francesco Acerbi kumewaimarisha
zaidi pamoja na kuwapata Nigel de Jong na Riccardo Montolivo.
Fiorentina wao waliweza kuwanasa Gonzalo
Rodríguez, Borja Valero, Facundo Roncaglia wa Boca Juniors, Alberto
Aquilani wa AC Milan na Luca Toni.
Uhamisho mwingine wa kuvutia ni kutua
kwa Mgiriki Sotiris Ninis Klabuni Parma akitokea Panathinaikos, Ederson
kwenda Lazio akitoka Lyon na mkopo wa Marco Borriello kwenda Genoa
kutoka AS Roma.
Germany
Bayern Munich, baada ya kuukosa Ubingwa
wa Bundesliga kwa Miaka miwili mfululizo ambao umekuwa ukinyakuliwa na
Borussia Dortmund, imebidi waingie sokoni kwa kishindo kujiimarisha na
wakamtwaa Mchezaji wa Spain Javi Martínez kwa Pauni Milioni 30 kutoka
Athletic Bilbao.
Kabla ya Martinez, Bayern Munich
waliwanunua Straika wa Croatia Mario Mandzukic, toka Wolfsburg kwa £11m,
Kiungo wa Uswisi Xherdan Shaqiri toka Basel kwa £10m na Beki wa Brazil
Dante Costa kwar £4m kutoka Borussia Mönchengladbach.
Wengine ni Claudio Pizarro alierudi tena
Bayern kwa Uhamisho wa bure kutoka Werder Bremen pamoja na Mitchell
Weiser na Tom Starke.
Wachezaji wa Bayern Munich waliohama ni
Ivica Olic, kwenda Wolfsburg, Danijel Pranjic kwenda Sporting Lisbon, na
Kipa Breno, alieachwa baada ya kuhukumiwa Kifungo cha Miaka minne na
Nusu Jela kwa kuchoma Nyumba moto.
Mabingwa Borussia Dortmund wao pia
hawakutulia bali waliwanunua Marco Reus, Leonardo Bittencourt, Julian
Schieber na Oliver Kirch.
Borussia Mönchengladbach walitumia £30m
kumnunua Alvaro Domínguez toka Atlético Madrid na pia kuwachukua Granit
Xhata wa Basel, Peniel Mlapa toka Hoffenheim, Luuk de Jong kutoka FC
Twente na Mchezaji wa Sweden Branimir Hrgota wa Jonkoping.
Wolfsburg waliwanunua Naldo wa Werder, Fragner Lemos wa Vasco de Gama, Bas Dost toka Heerenveen na Ivica Olic wa Bayern Munich.
Schalke wamemchukua Ibrahim Afellay toka Barcelona kwa mkopo pamoja na kuwabeba Tranquillo Barnetta wa Bayer Leverkusen.
Hamburga wao wamewapata Rafael van der Vaart wa Tottenham na Milan Badelj kutoka Dinamo Zagreb.
France
Paris Saint-Germain ndio walikufuru kwa
Ulaya nzima wakiwa na Fedha bwelele toka kwa Wamiliki wao wa Qatar
ambazo zimeweza kuwafanya waimarishe sana Kikosi chao.
Wachezaji waliotua kwa Matajiri hao wa
PSG ni Zlatan Ibrahimovic na Thiago Silva kutoka AC Milan kwa Dau la
£60m, Fowadi wa Argentina Ezequiel Lavezzi toka Napoli kwa £30m, Beki wa
kulia wa Holland Gregory van der Wiel toka Ajax kwa £5m na Mchezaji wa
Italia Marco kutoka Pescara kwa £10m.
Lyon, ambao siku zote wapo kwenye
kinyang’anyiro cha Ubingwa, hawakumnunua Kipa wa kumbadili Hugo Lloris
aliekwenda Tottenham lakini waliwanunua Beki wa Serbia Milan Bisevac
toka PSG na Kiungo Steed Malbranque kutoka Saint-Etienne.
Mabingwa wa France, Montpellie,
wamewanunua Straika wa Argentina Emanuel Herrera, Anthony Mounier,
Gaetan Charbonnier na Daniel Congre.
Kutua kwa Winga wa Chelsea Salomon Kalou hapo Lille ndio Uhamisho mwingine mkubwa kwenye Ligi 1.
Russia
Zenit Saint Petersburg ndio wajizatiti
sana kwenye Uhamisho kwa kutumia jumla ya Pauni Milioni 65 kuwanunua
Staa wa Brazil Hulk kutoka FC Porto na Kiungo wa Ubelgiji Axel Witsel
kutoka Benfica.
CSKA Moscow walimnunua Beki wa Brazil Mario Fernandes kutoka Gremio na Kiungo wa Sweden Rasmus Elm kutoka AZ Alkmaar.
Spartak Moscow wamewanunua Beki wa
kutoka Argentina Juan Manuel Insaurralde toka Boca Juniors, Mbrazil
Romulo Borges toka Grêmio, José Antonio Jurado toka Schalke na Kim
Kallstrom wa Lyon.
Klabu Tajiri Anzhi Makhachkala
haikufanya makeke kama yale ya kumnunua Samuel Eto’o lakini safari hii
wamejiimarisha kwa kuwachukua Mchezaji wa Ivory Coast Lacina Traoré toka
Klabu ya Urusi Kuban kwa £15m, Mbrazil Ewerton Almeida toka Corinthians
na Kiungo wa Real Madrid Lassana Diarra.
Nchi nyingine
Huko Portugal, Mabingwa FC Porto,
wamembadili Hulk kwa kumchukua toka Colombia mfungaji Jackson Martínez
wa Jaguares; Benfica imewabadili Witsel na Javi García kwa kuwabeba
Ernesto Cornejo toka Timu ya Vijana wa Barcelona na Straika wa kutoka
Brazil Rodrigo Lima wa Braga.
Sporting wao wamewanasa Khalid Boulahrouz, Gelson Fernandes, Daniel Pranjic, Marco Rojo na Martin Viola.
Huko Holland, Mabingwa Ajax imewapoteza
Van der Wiel, Jan Vertonghen (Spurs) na Mounir El Hamdaoui (Fiorentina),
lakini imewanasa Tobias Sana, Niklas Moisander na Christian Poulsen;
Feyenoord wamewaongeza Harmeet Singh, Lex Immens na pengine Joris
Mathijsen toka Málaga; Luciano Narsingh amejiunga PSV na Wachezaji
Steven Berghius, Donny Gorter, Yves de Winter and Markus Henriksen wapo
Alkmaar.
Olympiakos ya Greece imekaribisha
Wachezaji kadhaa wakiwemo yule wa AS Roma, Leandro Greco, toka Toulouse
ni Paulo Machado, Pablo Contreras wa Colo-Colo na Vasssilis Karagounis
wa Udinese. Wapinzani wao, Panathinaikos, wamempoteza Ninis, lakini
wamewanasa Bruno Fornaroli toka Sampdoria, Quincy Owusu-Abeyie na Pape
Habib Sow.
Comments
Post a Comment