UFARANSA-HATUTA VUMILIA MAANDAMANO YA AINA YOYOTE HARAMU

Serikali nchini Ufaransa imesema haitavumilia maandamano yoyote haramu kuhusiana na filamu ya Marekani iliyokejeli dini ya kiisilamu na Mtume Muhammad.

Maafisa wa utawala nchini humo pia wana wasiwasi ya taharuki miongoni mwa waisilamu heunda ikachochewa zaidi na vikatragosi vilivyopchhorwa katika jarida moja nchini humo.
Vikaragosi hivyo vinawafanyia mzaha waisilamu walioandamana na kuzua vurugu wiki jana wakilaani filamu ya Marekani dhidi ya uisilamu
Mwandishi wa BBC anasema kuwa mitandao ya kijamii imejaa taarifa za kuwataka waisilamu kufanya maandamano mjini Paris
Marseille na katika miji mingine nchini humo.
Ulinzi umedhibitiwa katika balozi na shule za ufaransa katika nchi 20. Viongozi wa kiisilamu nchini humo wamewataka waisilamu kuwa watulivu huku wakilaani mtu aliyechora vibonzo hivyo.

Comments