
Takriban watu 26 wameuawa Kaskazini mwa Mexico baada ya mlipuko na kisha moto kuzuka katika kiwanda cha gesi katika jimbo la Tamaulipas.
Kampuni ya mafuta ya serikali ya Mexico,Pemex imeeleza kwamba moto huo ulitokea katika kiwanda hicho nje ya Reynosa iliyo karibu na mpaka na Marekani.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, Juan Jose Suarez, alisema kuwa watu ishrini na tano wlaiuawa katika kiwanda hichho huku mmoja akikanyagwa na gari.
Wafanyikazi wengine wengi walijeruhiwa.
Akizungumza katika mkutano na waandishi habari, Juan Jose Suarez Coppell alisema kuwa tayari wameanzisha uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha mlipuko huo
Visa kama hivyo, vimewahi kutokea katika viwanda vilivyoko karibu vya Pemex katika miezi miwili iliyopita ambavyo vimesemekana kutokea kutokana na wizi wa mafuta unaotekelezwa na makundi ya wahalifu.
Comments
Post a Comment