Skip to main content
SERIKALI YA MAURITAINIA YAWAKABIDHI LIBYA, MKUU WA UJASUSI
Serikali ya Mauritania imewakabidhi maafisa wa utawala wa Libya aliyekuwa mkuu wa ujasusi nchini humo, Abdullah al-Senussi.
Libya inataka kumfungulia mashtaka bwana Senussi kwa makosa aliyoyafanya chini ya utawala wa hayati Muamar Gaddafi.
Mapema mwezi huu rais wa Mauritania,
Mohamed Ould Abdel Aziz alisema kuwa bwana Sanusi aliyekuwa amekimbilia
nchini humo, sharti kwanza akabiliwe na sheria kwa makosa ya kuingia
Mauritania kinyume na sheria.
Senussi alitoroka Libya baada ya mapinduzi ya mwaka jana ambayo yalimng'oa mamlakani Muammar Gaddafi.
Pia anatakiwa na Ufaransa pamoja na mahakama ya kimataifa kuhusu haki za bianadamu ICC kwa makosa ya kukiuka haki za binadamu.
Ripoti za kukabidhiwa kwake kwa watawala wa
Libya, zilitolewa na televisheni ya taifa pamoja na shirika rasmi la
habari la Mauritania.
Kulingana na ripoti, bwana Senussi alikabidhiwa
kwa wajumbe wa Libya walioongozwa na waziri wa sheria na haki wa nchi
hiyo. Lakini hadi sasa bwana Senussi hajulikani aliko.
Comments
Post a Comment