
Kitengo cha umoja wa mataifa kinachochunguza matumizi ya zana za nuclear IAEA, kimeanza mkutano wa bodi yake, ambapo inatarajiwa kuwa Iran itashutumiwa kuhusu mpango wake wa zana za kinuclear.
Katika kielelezo ambayo BBC iliiona Marekani, Uingereza, China, Ufaransa, Ujerumani na Urusi zimeelezea wasiwasi mkubwa kuhusu shughuli za Iran za kutengeneza madini ya Uranium.
Mwandishi wa BBC amesema hatua hiyo ya mataifa hayo sita yenye uwezo mkubwa duniani ni kuonyesha umoja wakati Israel ikidokeza kuwa kuna uwezekano wa kuishambulia Iran.
Comments
Post a Comment