
Walimu mjini Chicago wamepiga kura kusitisha mgomo wao ambao umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya wiki moja na kusababisha shule kufungwa mjini humo.
Mgomo huo mbao ulikuwa wa kwanza kufanyika katika kindi cha miaka 25, ulilenga kupinga mageuzi yanayofanywa katika sekta ya elimu mjini humo.
Mageuzi hayo yalipendekezwa na meya wa mji Rahm Emanuel.
Mgomo huo wa walimu umeonekana kama aibu kubwa kwa rais Barack Obama wakati huu wa kampeini za uchaguzi wa urais.
Comments
Post a Comment