MGOGORO WA CHINA NA JAPAN WASABABISHA BAADHI YA MAKAMPUNI YA JAPAN KUFUNGWA UKO NCHINI CHINA

Makampuni kadhaa ya Japan yamesitisha shughuli zao nchini China baada ya siku kadhaa za maandamano dhidi ya Japan kuhusiana na mzozo wa umiliki wa kisiwa wanachozozania.
Kampuni za Panasonic na Canon zimefunga viwanda vyao baada ya kuporwa huku wafanyabiashara wengine wa Japan wakishambuliwa wakati wa maandamano.
Gazeti la chama rasmi cha kikomunisti, The Peoples' Daily, limeonya kuwa Japan huenda ikaathirika kibiashara ikiwa itaendelea na kile kilichotajwa kuwa uchokozi wake kuhusiana na kisiwa hicho kilicho Mashariki mwa China.
Japan imeonya wananchi wake dhidi ya kufanya maandamano siku ya Jumanne , ambayo itakuwa siku ya maadhimisho ya utawala wa Japan Kaskazini Mashariki mwa China mnamo miaka ya thelathini.

Comments