MENEJA NEW CASTLE AFUNGIWA MECHI MBILI

Meneja wa Newcastle Alan Pardew amefungiwa na Chama cha Soka England, FA, Mechi mbili na kupigwa Faini ya Pauni 20,000 baada ya kukubali kosa la utovu wa nidhamu kufuatia tukio kwenye Mechi ya Agosti 18 Newcastle walipocheza na kuifunga Tottenham bao 2-1 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.

Katika Mechi hiyo, Alan Pardew aliondolewa kwenye Benchi la Ufundi kwa Kadi Nyekundu na Refa Peter Kirkup alipolalamikia kuwa mpira umetoka nje na kwa ghadhabu akamsukuma Refa Msaidizi.

Adhabu hii ya Pardew inaanza mara moja na atalazimika kukaa kwenye Jukwaa la Mashabiki Newcastle watakapocheza na Everton na kufuatia Mechi na Norwich City kwenye Mechi za Ligi Kuu.

Comments