Televisheni ya taifa nchini humo iliripoti kuwa mabomu mawili yalilipuka, moja likilipukia ndani ya makao hayo.
Inaarifiwa kuwa waasi walifyatua risasi bado wakiwa ndani ya makao hayo ya jeshi.
Walioshuhudia tukio hilo walielezea kusikia ufyatulianaji risasi kwa masaa kadhaa ingawa duru za kijeshi zilisema kuwa hakuna mwanajeshi aliyejeruhiwa katika mashambulizi hayo.
Mwandishi wa gazeti la Sunday Times katika mji huo anasema milipuko miwili ilitangulia na kufuatiwa na mashambulio zaidi kutoka kwa vikosi vya waasi, ikiwemo makombora kabla ya makao hayo kuteketezwa moto.
Wanaharakati wanaopinga serikali, wameripoti kutokea vifo pande zote mbili.
Mwandishi habari wa kituo cha televisheni cha Iran Press Tv, aliuawa kwenye shambulio hilo. Duru za kidiplomasia zinasema kuwa maafisa wa usalama wamekuwa wakifanya msako wa nyumba hadi nyumba kuwakamata wale waliohusika na shambulizi hilo.
Comments
Post a Comment