Skip to main content
MAHARAMIA WAITEKA MELI YA MAFUTA HUKO NIGERIA
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la wanamaji nchini Nigeria, Jerry
Omodara, haijulikani iliko meli hiyo na kwamba juhudi za kuitafuta
zinaendelea.Shirika la kimataifa la mabaharia, liliambia shirika la habari la AFP
kwamba mabaharia 23 walikuwa kwenye meli hiyo wakati ilipotekwa na
walikuwa wamejifungia ndani ya chumba kimoja salama wakati wa tukio
hilo.
Wadadisi wanasema kuwa visa vya uharamia vimekithiri katika maeneo mengi ya Afrika Magharibi.
Shirika la kimataifa la mabaharia, linasema
liliweza kurekodi visa kumi na saba vya utekaji nyara wa meli nchini
Nigeria, katika miezi ya kwanza sita ya mwaka huu. Linasema kumekuwa na
ongezeko kubwa la visa hivyo ikilinganishwa na mwaka 2011.
Mkuu wa kituo cha shirika hilo cha kuripoti visa
vya uharamia nchini Malaysia, Noel Choong, amesema kuwa wale waliofanya
kitendo hicho, huenda ni kundi moja la maharamia walioteka nyara meli
za mafuta nchini Togo mwezi jana, kuiba mafuta na baadaye kuwaachilia
mabaharia waliokuwa kwenye meli hiyo.
Luteni Omodara anasema kuwa helikopta moja inatumiwa kuisaka meli hiyo katika juhudi za kuikoa.
Mwaka jana Nigeria na nchi jirani ya Benin zilianza mpango wa pamoja wa kuweka usalama baharani ili kupambana na uharamia.
Comments
Post a Comment